Saturday, March 31, 2018

NGUVU YA KUWEKA NA KUFANIKISHA MALENGO

1.FOCUS KWENYE LENGO MOJA


Watu wengi tuna kasumba ya kutaka mambo mengi katika wakati mmoja na hii husababisha kuto fanikiwa . tengeneza time frame kwamba jambo fulani lita takiwa kufanikiwa kwa muda fulani na hii sio yale malengo makubwa katika ya maisha haya ni malengo madogo madogo. tafuta lengo moja utakalo kuwa commited nalo ili ufanikishe kwa kipindi ambacho utaweza fanikisha

je lengo lako litakuwaje? chukua muda kaa tafakari ni wapi unataka kuwa au kufanikiwa kuanzia sasa, andika kwenye ki daftari chako .. kisha fuatilia sasa tilia mkazo

2.TENGENEZA MALENGO MADOGO MADOGO
katika lile lengo moja unalo litaka , livunje vunje kwenda kwenye malengo madogo madogo ma nne, kisha kama lengo lilikuwa lina kuchukua mwaka basi tengeneza vi lengo lengo vidogo alafu uanze kutimiza yale malengo madogo madogo  moja baada ya mengine ambapo yatakua sogeza kwenye lengo kubwa.

3.JIULIZE KWA NINI/KWA VIPI UTAFANIKISHA
orodhesha mahitaji ya kukusaidia kutimiza malengo, na sababu za kwa nini ufanikiwe kwenye hilo lengo, je utahita pesa ili ufanikiwe?,research, mentorship emotional support n.k utahitaji nini ili utimize lengo

note:hata kama ni hitaji dogo namna gani, usilidharau na kusema utakumbuka li note

4.CHAGUA VIPAUMBELE VYAKO
ukitambua vipaumbele vyako vitakusaidia katika safari ya mafinikio. sasa umeshatengeneza malengo yako na umesha jua unahitaji nini ili ufanikiwe sasa katika orodha yako kuna vya muhimu na ambavyo sio muhimu, ukiangalia utaona vya haraka vya kufanya na ambavyo havina haraka vitengee na uvitekeleze


5. TENGA MUDA KWA WIKI
sasa umesha kuwa na vipaumbele hakikisha  katika wiki tenga japo siku mbili na masaa kadhaa ili kufanikisha lengo moja, nimekuambia utenge siku 2 sababu uwe commited na jambo moja baada ya jingine na ukitenga siku mbili , tambua siku moja inaweza kukutosha na nyingine ni back up tu.

kumbuka lengo lako ni kutengeneza tabia ya kila siku itakayo kufanya ufanikiwe katika lile lengo lako kubwa
kwa muda wowote utakao tenga , hakikisha unaweka alarm ya kukumbusha, waambie wale ambao wata kuwa chanzo kama familia, marafiki kuwa utakuwa busy muda fulani ili wasikusumbue ..,
 kuwa mvumilivu kuwa commited


6. CHUKUA HATUA YA KWANZA
ndio, sasa hivi chukua hatua. umepata muda wa kusoma ujumbe huu , unao muda wa kutenga lengo moja na kuli chambua katika makundi ma tatu, muda ni sasa.  usisubiri kupanga sijui kesho au lini hatua kati ya ulipo na unapo kwenda ni kuamua kuanza sasa.



hizi hatua sita ni siri ya kufanikisha chochote kile unachotaka

No comments:

Post a Comment