HATUA 10 ZA KUFUATA KABLA YA KUFUNGUA
BIASHARA .
Uamuzi wa kufungua Biashara , unaweza kuwa moja ya uamuzi wenye kuchanganya katika maisha yako kwani huwa na changamoto nyingi. Ila kuna vitu vingi vya kufuta kwa kupitia hatua mbali mbali zenye gharama na zisizo na gharama ili ufikie unapotaka.
Zifuatazo ni hatua 10 zitakazo kusaidia katika safari ya kuanzisha biashara yako. Pitia hatua moja baada ya nyingine ili umiliki biashara yako.
HATUA 1. HAMASIKA
Kila biashara huanza katika WAZO. Unawea ukawa umewaza na kuota mara nyingi kuanza biashara yako kwa miaka mingi, au umehamasika kwa ghafla baada ya kuona mtu au changamoto fulani. Hatua ya kwanza ya kuanza biashara anza na WAZO .
HATUA 2. FANYA UTAFITI
Umesha hamasika kwa kuwa na wazo , sasa ni muda wa kuliweka sawa wazo lako kiuhalisia. Upo tayari kuanza biashara embu fuata hii quiz ndogo hapa chini ili ujichunguze mwenyewe kama unaweza kuimiliki hiyo biashara yako.
Ili kuwa na biashara yenye mafanikio, unatakiwa uanze kwa kusuluisha tatizo fulani, angalia nini kinahitajika kwa wakati huo na wewe ulipatie ufumbuzi. Kuna njia tofauti za kusulihisha mfano angalia mtaani kwako,au. Majirani wanahitaji nini kwa muda huo kisha uwape solution ambayo watailipia ambapo ni biashara.
Je hicho unachotaka kuuza kinahitajika kwa muda huo?? Au unauza ili na wewe uwe miongoni mwa wanao uza??
Je nani ana hitaji hiyo bidhaa unayotaka kuuza?
Je kuna watu wengine wanafanya hicho unacho taka kukifanya sasa, kama ndio jua wanakosea wapi na huduma yao ipoje (itakusaidia kujua wewe upunguze au kuongeza wapi)
Ushindani wako upo je??
Biashara yako ita FIT vipi sokoni?
Usisahau kujiuliza maswali pia kuhusu kuanzisha biashara yako.
HATUA 3. MPANGO (plan)
Unahitajika kutengeneza mpango biashara wa lile WAZO lako uliloligundua. Utafute msaada na Ushauri wa kifedha tokea kwa taasisi za kifedha na waliopiga hatua zaidi yako.ili uweze kuwa na MPANGO BIASHARA (business plan) wenye kuleta mafanikio.
Hata kama utashindwa kupata msaada kwenye taasisi za kifedha basi wewe andika chini ni kwa vipi ungependa kufanikiwa na upange utafanikiwa vipi.
Kwa ujumla andaa katika maandishi, mafanikio unayo yataka na motisha nyuma ya mafanikio ya malengo ya kufanikiwa katika mpango wako wa kufikia malengo na soko lako.
HATUA 4: MPANGO FEDHA
Kuanzisha biashara hizi ndogo ndogo hakuhitaji kiasi kikubwa cha fedha , ila unahitajika kuwekeza zaidi, kuna hatua mbali mbali za kukuza biashara yako katika mifuko mbali mbali.
- Kama vile
- Mikopo midogo midogo
- Vicoba
- Wawekezaji.
Wewe mwenyewe kama unaweza jipatia mtaji pia unaweza anza biashara ila uweke mpango pesa wa pesa zako pia ili usije kula mtaji wako
HATUA 5: CHAGUA MUUNDO WA BIASHARA
biashara yako hiyo hiyo ndogo unayo ianzisha inaweza kukuletea washika dau tofauti inaweza ikawa na limited liability company (LLC) au hata chama cha biashara. Muundo wa biashara utakao chagua utaleta matokeo katika jina lako la biashara , katika mapato yako, na hata katika kuandaa maswala ya kodi
Unaweza tengeneza muundo wa biashara yako ndogo na ukiutumia vizuri siku zitakavyo enda utagundua kuwa haukutoshi hapo ndipo utakapo jua biashara yako inakua.
HATUA 6: CHAGUA JINA LA BISHARA NA LISAJILI.
Jina lako la biashara lina nafasi kubwa na muhimu sana katika nyanja tofauti za biashara kwa hiyo tafuta jina zuri .
Unapokuwa umechagua jina la biashara yako, hakikisha linakuwa chapa yako kama unavyosikia BAKHRESA, IPP MEDIA N.K. BRELA ndio wanao husika na usajili wa jina la biashara
HATUA 7: VIBALI NA LESENI
Hakikisha una vibali na leseni zinazo kuruhusu wewe kuendesha biashara hiyo , laa si hivyo utakuwa unafanya biashara kienyeji na itaweza kukusababishia kuingia mikononi mwa sheria.
HATUA 8: ENEO LA BIASHARA
Kuandaa eneo la biashara ni muhimu kwa utekelezaji wa biashara yako, kama itakuwa nyumbani au ofisini, uta share au itakuwa binafsi ya kwako au utakodisha NI MUHIMU.
Fikiria eneo la kuendeshea biashara , vifaa na hakikisha hilo eneo unalo anzisha biashara watu wa hapo wanahitaji huduma hiyo.
HATUA 9: UTAALAMU WA PESA (uhasibu)
Jambo la muhimu kabisa katika biashara ni kuwa na system nzuri ya utaalamu wa pesa.
Ni muhimu ili kutengeneza bajeti, kulipa kodi,kujua faida, kupanga malengo yako, kama huwezi kuwa mtaalamu wa pesa za biashara yako ili ikue na iwe yenye mafanikio ni bora uajiri muhasibu kabisaaaa.
HATUA 10: TANGAZA BIASHARA YAKO
Biashara hii ikiwa imesha simama na inaendelea, chukua hatua ya kuanza kuvutia wanunuzi, au wateja. Andaa mpango wa soko lako unavyo taka liende kwa kujumlisha discounts,offer n.k
Chagua jinsi ya kuhakikisha unatangaza biashara yako na unaikuza kwa matangazo, unaweza ukawa huna pesa ya matangazo kwa sasa ila utakavyo mpa huduma nzuri mteja mmoja jua atarudi na wateja 3 .
Utakapo kamilisha hatua hizi za biashara utakuwa na moja ya biashara ndogo na yenye umuhimu kuwa tayari
Thank me later
No comments:
Post a Comment