Friday, April 6, 2018

FALSAFA YA MAISHA AWAMU YA 2...USIOGOPESHWE NA MAFANIKIO YA WENGINE


kuna mtu ana graduate akiwa na miaka 21 na hakupata kazi mpaka alipo fikia miaka 27

kuna baadhi ya watu wakiwa na miaka 25 walichelewa ku maliza masomo ila walipata kazi haraka mno 

tunawajua baadhi ya watu ambao hawajafika chuo kikuu ila wamefanikiwa kutoboa kimaisha wakiwa na miaka 18.

kuna mtu yeye alipo maliza shule /chuo ali pata ajira papo kwa hapo na isitoshe ana kazi inayo muingizia pesa nyingi na nzuri ila kazi anayo ifanya ,   kazi anayo ifanya haipendi .


baadhi ya wenzetu  wamechukua miaka mingi toka wamalize shule  bila kufanya lolote na bado wamefanikiwa kujua dhumuni lao la kuishi wakafanikiwa.


kuna baadhi walikuwa na hakika ya nini wana kitaka wakiwa na miaka 16, wakabadilisha mawazo  wao wakiwa na miaka 26.

kuna baadhi ya watu ambao ni wa pweke katika mahusiano (single) ila wana watoto

na kuna baadhi ya watu ambao wameolewa zaidi ya miaka 7,10 n.k na hawana watoto

kuna watu wapo katika mahusiano ila kila mmoja anampenda mtu mwingine, huku wengine wanapendana ila hawawezi kuwa pamoja.

katika maisha kila jambo linatokea kutokana na  muda wetu .

unaweza ogopeshwa na hatua za mafanikio marafiki na ndugu ulio zaliwa nao , ulio cheza nao utotoni, ulio soma nao walizo piga mbele yako ukaanza kupaniki na kuchanganyikiwa, au ukaona wengine wapo nyuma yako kimaendeleo. tambua kuwa muda wao haujafika au muda wao wa mafanikio waliyo kutangulia umesha wapitia.


KUWA MVUMILIVU, USIIGE NA WALA USI HARAKISHE NA PIA USI NUNG'UNIKE

No comments:

Post a Comment