Tuesday, April 3, 2018

FALSAFA 18 ZA MAISHA









1. Mwenye saa moja ukimuuliza muda atakutajia sawa sawa - mwenye saa mbili ukimuuliza muda  hatokuwa na hakika


 2. Usikae chini ukaangalia ulipo shindwa - angalia ulipo teleza.




3. Angalia maisha unayo ishi katika wind-shield(kioo kikubwa kinacho zuia upepo katika gari) na sio rear mirror(kioo cha nyuma kinacho , kitumikacho kuangalia ya nyuma katika gari)



4. Hakuna mahali utakapo pata Amani kama si kwako mwenyewe- hata kwa sangoma hakuna.



5. Binadamu wata kuwekea mashaka kwa yale unayosema - wataamini utakayo fanya tu.

6. Kuwa mwema kwa walio chini  wakati unaelekea juu  - utawahitaji siku utakapo shuka chini.

7. Muda ulio furahia kuupoteza -haukupotea ( muda haupotei)




8.usijielezee sana kwa marafiki hawaitaji maelezo yako - maadui hawatokuamini pia. (Fanya unavyo weza)

9. Unapo panga kulipa kisasi chimba makaburi mawili - moja lako


10. Ujasiri sio kukosa woga - uwezo kutenda unapokutana na woga.

11. Jitahidi kukua bila kujali kupita urefu wa baba yako ni kiasi gani.

12. Njia nzuri ya kutabiri mambo yako yajayo ni kujenga sasa hivi.

13. Ni bora kuchukiwa kwa jambo ulilo nalo kuliko kupendwa kwa jambo usilo nalo.

14. Usijali juu ya uliokuwa nao kipindi cha nyuma , ni sababu pekee ya kwa nini haupo nao sasa hivi- usijute

15. Furaha ni faida kuliko utajiri- hakuna anayeweza kukuazima







16. Kila jambo hutokea kwa sababu

17. Msamaha sio kitu unafanya kwa ajili ya uliye mkosea- unasamehe  ili uwe huru na uweze kusonga mbele wewe binafsi.

18. Tofauti unayo iona baina yako na mwingine ndio uzuri wako 





3 comments: